TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI - HALI YA HAKI ZA BINADAMU KWA KIPINDI CHA
NUSU MWAKA
JANUARI
– JUNI 2014
Ndugu
waandishi wa habari
Kituo
cha Sheria na Haki za Binadamu, kinaendeleza utaratibu wake wa kila
mwaka wa kutoa tathmini ya hali ya haki za binadamu kwa kipindi cha
miezi sita. Tathmini hii hufanywa kwa malengo ya kutoa muelekeo wa
hali ya ulinzi na ukiukwaji wa haki za binadamu.
Taarifa
hizi ni matokeo ya tafiti mbalimbali zilizofanywa na Kituo cha Sheria
na Haki za Binadamu, ufuatiliaji wa ukiukwaji wa haki za binadamu,
pia taarifa mbali mbali toka kwa waangalizi wa haki za binadamu,
wasaidizi wa kisheria, taarifa rasmi toka taasisi za Serikali, Bunge,
Mahakama, vyombo vya habari na asasi mbali mbali zisizo za
kiserikali.